Tuesday, 30 June 2015

Chadema wafurika kurudisha fomu za ubunge

Katibu wa Chadema Ofisi ya Kanda ya Pwani, Halfan Milambo akipokea fomu za mtangazania ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Ilala kupitia chama hicho, Joyce Charles (katikati) huku akimpongeza kwa kurudisha fomu hizo Dar es Salaam jana. 

Makada mbalimbali wa Chadema jana walirudisha fomu za 
Inaendelea.......

Monday, 15 June 2015

Kumekucha Korogwe Mjini.

CCM HAWANA SULUHISHO LA MATATIZO YETU KWA MIAKA 50 SASA WASITUDANGANYE WATAKUJA NA SULUHISHO OCTOBER 2015. TATIZO LETU KUBWA 
NI CCM NA WAGOMBEA WAO TUWAKATAE KATIKA SANDUKU LA KURA  2015.  

Njiani Kuelekea frontline Kulia Ni Kamanda Steve Kimea ambae ndie Mgombea Ubunge
 Jimbo la Korogwe Mjini.
 
Vijana Bavicha Korogwe mjini wakimsikiliza Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini
Kamanda Steve Kimea wakimfatilia kwa Makini.
 Mkutano wa Bavicha Jimbo la Korogwe Mjini.
Mgombea Ubunge Jimbo La Korogwe Mjini Kamanda Kimea, akibadilishana  Mawazo na Kamanda Katika  jimbo la Korogwe vijijini

Thursday, 11 June 2015

Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini

Ndugu Steve Kimea 
Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Kwa Chama Cha Democrasia Na Maendeleo Chadema ambaye ni Tumaini jipya la wana Korogwe mwenye dhamiri ya dhati katika kuleta mabadiliko katika jimbo la Korogwe Mjini. Na kuanzia Tarehe 18/06/2015. Ni tarehe za kujiandikisha kupiga kura kwa wakazi wa Manundu, Kilole,Old Korogwe, Mtonga, Kwamsisi, Mgombezi,kwandolwa na magunga. Napenda kuchukua fursa hii kukusihi Mwana Korogwe mwenzangu ujitokeze kwa wingi kuandikishwa katika vituo ambavyo vitategwa kumbuka ni haki yako ya muhimu itakayo leta mabadiliko ya kiuchumi na kimaendeleo.Hivyo utakapo sikia mtaharifu na mwenzio ili mtu hasikose kushiriki haki hii ya msingi kwa kila mwana Korogwe Mjini na wananchi wote kwa ujumla. Haki hii inawahusu wale wote wenye sifa na waliotimiza umri wa miaka 18 na watakaofikisha umri wa miaka 18 ifikapo mwenzi Octoba.


Friday, 5 June 2015

Lissu, Aponda Safari ya Matumaini ya Lowasa, adai ni ya Matumizi".

Na Bryceson Mathias, Dodoma.

MWANASIASA Machachari na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni,Tundu Lissu, ameponda Safari ya Matumaini ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, akidai si ya Matumaini, ni ya Matumizi.

Lissu alisema hayo jana katika Mkutano wa Hadhara alioufanya mkoani Dodoma katika Viwanja vya Barafu, ambapo pia alidai Watawala hao hawana uwezo tena wa kutawala kama kwanza.

Inaendelea.......

Thursday, 4 June 2015

Wanachama Wapya Waliochukua Kadi Ya Uwanachama

Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini Ndugu Steve Kimea akiwa na wanachama wapya waliochukua kadi ya uwanachama wa Chama Cha Democrasia Na Maendeleo Chadema.Hizo ni moja wapo kati ya majukumu ya mgombea huyo katika kuwaelimisha wananchi wa Korogwe mjini na katika Mitaa, vijiji na vitongoji, mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko.
 Safari ya amani na upendo ndani ya Korogwe Mjini mpaka kieleweke 2015.


Monday, 1 June 2015

NI MUHIMU: KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KOROGWE.

Kuanzia tarehe 18/06/2015. Ni tarehe za kujiandikisha kupiga kura kwa wakazi wa Manundu, Kilole,Old Korogwe, Mtonga, Kwamsisi, Mgombezi,kwandolwa na magunga. Napenda kuchukua fursa hii kukusihi Mwana Korogwe mwenzangu ujitokeze kwa wingi kuandikishwa katika vituo vyitakavyokuwepo karibu na eneo unapoishi. Nakusihi kutumia fursa hii Muhimu kwa wote wenye umri wa kupiga kura na wale wanaotarajia kufikisha umri wa miaka 18 ifikapo mwezi wa kumi mwaka Huu. Kumbuka Kuwa Mwaka Huu ni mwaka wa mabadiliko tukatae. Rushwa ya Kanga,pesa na vitenge ili utu wetu uthamaniwe.

********************************************************************************************************************
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MHE. SUSAN ANSELM JEROME LYIMO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016
Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili, 2013
_______________________
1.   UTANGULIZI
Mheshimiwa spika, napenda kuchukua fursa hii adhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema na kuweza nkusimama hapa kusoma hotuba hii.   Kipekee namshukuru sana Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mhe. Freeman Mbowe kwa kuendelea kuniamini katika kusimamia Wizara hii nyeti kwa maendeleo ya Taifa. Aidha, nawapongeza kwa dhati wenyeviti wenza wa UKAWA; Mhe. Dkt. Emanuel Makaidi wa NLD, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF na Mhe. James Mbatia wa NCCR Mageuzi kwa kazi kubwa sana na nzuri  wanayofanya  ya kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na UKAWA kwa kuwa ndio tumaini pekee  lilobaki la kuwakomboa na ndio njia pekee ya kuiondoa serikali  ya CCM madarakani ifikapo 25/10/2015. Hivyo naomba wananchi wote wanaokerwa na kuporomoka kwa shilingi yetu, ufisadi, rushwa na hali mbaya ya maisha watumie fursa hii ya maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kujitokeza kwa wingi na kuwahi kujiandikisha mapema daftari litakapopita katika maeneo yao kwani ndio njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani kidemokrasia.
Inaendelea.......

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROAD SLAA MKOANI RUKWA

Inaendelea.......