Monday 1 June 2015

MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROAD SLAA MKOANI RUKWA

Inaendelea.......
wakimsindikiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad Slaa baada ya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji huo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ndua. Barabara za mji huo zililazimika kufungwa kwa muda na shughuli kusimama wakati wananchi wakiwa katika shamrashamra ya kumsnikiza kiongozi huyo ambaye yuko katika ziara ya kikazi kukagua uandikishaji wapiga kura kwa BVR, kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwa wingi huku pia akikagua maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.



MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR WILBROAD SLAA MKOANI KATAVI 

Msafara wa pikipiki na magari mjini Katavi leo wakati wanachama, mashabiki, wapenzi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walipojitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibroad Slaa ambaye yuko kwenye ziara ya mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR, kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa wingi kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura huku pia akikagua maandalizi ya chama kwenda kushinda uchaguzi mkuu mwaka huu.


DR WILBROAD SLAA ATEMBELEA KUKAGUA ZOEZI LA UWANDIKISHAJI WANANCHI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA MKOANI MBEYA
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk, Wilbroard Slaa , akizungumza na wananchi waliojikeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga katika kijiji cha Igamba wilayani Mbozi jana.

 

No comments:

Post a Comment