Wednesday 9 September 2015

LOWASSA ATIKISA KIBAMBA DAR

 Mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda UKAWA, Mh. Edward Lowassa, leo tena amelitikisa jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya Kibamba kulikofanyika mkutano wa kihistoria wa kampeni ambapo maefu ya wananchi walifurika wengine wakikaa juu ya mapaa ya nyumba za madarasa, wengine kwenye miti, kutokana na kukosa eneo zuri la kuweza kushuhudia "live" mkutanonukiendelea. Changamoto ya maeneo ya kufanyia mikutano ya kampeni ndiyo inayoonekana kuikumba UKAWA, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo. Pichani mfuasi wa UKAWA, akiwa amejichora rangi za bendera ya CHADEMA akiambatanisha maneno maarufu yanayotumiwa na wafuasi wa Mh. Lowassa kwa sasa, yaani "Ulipo tupo".
 Mh Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa Chadema Bara Mh John Mnyika katika mkutano uliofanyika jimboni Kibamba.






Monday 7 September 2015

MAPOKEZI MAKUBWA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA MKOANI KIGOMA

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Jimbo la Kigoma Kusini, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.



 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Kigoma Kusini, waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.

 Baadhi ya wananchi wa Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.Picha na Othman Michuzi, Kigoma.


Thursday 3 September 2015

MKUTANO WA EDWARD LOWASSA SUMBAWANGA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Ikuo Malila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akizungumza wakati akitolea taarifa swala na ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa (kushoto) uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015.

 Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Sumbawanga, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, wakiishangilia Ndege iliyombeba Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili Uwanjani hapo, leo Sepremba 2, 2015.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa, wakiwapungia mikono maelfu ya wananchi wa Sumbawanga Mjini, waliofurika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, leo Sepremba 2, 2015.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015.

Wednesday 2 September 2015

JUMA DUNI AHUTUBIA WAKAZI WA MTWARA




MAPOKEZI MAKUBWA YA EDWARD LOWASSA SONGEA

Picha Chini: Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Songea Mjini, kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015. Picha na Othman Michuzi, Ruvuma.





Tuesday 1 September 2015

MAPOKEZI YA EDWARD LOWASSA NJOMBE MJINI

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya Shirika la Nyumba (National Housing) Mjini Njombe tayari kwa kuhutubia Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, anazoendelea kuzifanya kwa nchi nzima. Picha zote na Othman Michuzi, Njombe.




Monday 31 August 2015

LOWASSA AUNGURUMA IRINGA

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao kupata faida yoyote.

Lowassa alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.

Lowasa ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini Mafinga.

Lowassa alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura kwasababu ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi na maneno hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.

“Mimi nataka kila mtu akihifazi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura zenu” alisema Lowassa

Katika mkutano huo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai alipanda jukwaani na kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chadema, William Mungai ambaye ni mtoto wake.

Mungai aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na aliweza kuteuliwa nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.

Mungai alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William Mungai kwa sababu mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo hakuweza kuongoza kama alivyofanya yeye.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, William Joseph Mungai, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.
 Waziri wa zamani wa Elimu, Mh. Joseph Mungai akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015.
 Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa leo Agosti 30, 2015
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsalimia kijana mwenye ulemavu (jina lake hakupatikana kwa haraka) aliyehudhulia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Iringa Mjini, leo Agosti 30, 2015.Picha na Othman Michuzi, Iringa.

 Umati wa Wakazi wa Mji wa Iringa Mjini ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Agosti 30, 2015