Wednesday, 9 September 2015
LOWASSA ATIKISA KIBAMBA DAR
Mgombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda UKAWA, Mh. Edward
Lowassa, leo tena amelitikisa jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya
Kibamba kulikofanyika mkutano wa kihistoria wa kampeni ambapo maefu ya
wananchi walifurika wengine wakikaa juu ya mapaa ya nyumba za madarasa,
wengine kwenye miti, kutokana na kukosa eneo zuri la kuweza kushuhudia
"live" mkutanonukiendelea. Changamoto ya maeneo ya kufanyia mikutano ya
kampeni ndiyo inayoonekana kuikumba UKAWA, kutokana na kuongezeka kwa
idadi ya watu wanaohudhuria mikutano hiyo. Pichani mfuasi wa UKAWA,
akiwa amejichora rangi za bendera ya CHADEMA akiambatanisha maneno
maarufu yanayotumiwa na wafuasi wa Mh. Lowassa kwa sasa, yaani "Ulipo
tupo".
Mh Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa Chadema Bara Mh John Mnyika katika mkutano uliofanyika jimboni Kibamba.
Mh Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba ambaye pia ni Naibu katibu mkuu wa Chadema Bara Mh John Mnyika katika mkutano uliofanyika jimboni Kibamba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment