Friday, 28 August 2015
Thursday, 27 August 2015
Uchaguzi Mkuu 2015: Serikali Yapiga Marufuku Kutumia Helikopta Wakati wa Kampeni Bila Kibali
- UTANGULIZI
- Tangazo
hili linatolewa kwa lengo la kutoa mwongozo kwa watoa huduma za
helikopta, marubani wake na umma kwa ujumla kuhusiana na hatua za
kiusalama zinazopaswa kuzingatiwa inapolazimika kutoa huduma ya usafiri
wa helikopta hapa nchini, hususan, maeneo ya mbali (vijijini) ambapo
huduma za uongozaji ndege hazipo au sio maeneo maalum yaliyotengwa kwa
ajili ya helikopta kutua (mahsusi kwa helikopta au viwanja vya ndege kwa
ujumla). Tangazo hili limetolewa baada ya Mamlaka
kugundua kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya huduma hizi kinyume na
kanuni za usafiri wa anga nchini na weledi unaozingatia taratibu za
kitaaalamu na miongozo katika usafiri wa anga.
. - Mamlaka inatambua kwamba matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yanatarajiwa kuongezeka na kuna uwezekano wa kuleta athari za kiusalama kwa maisha ya watu na mali pamoja na watumiaji wa vyombo hivi. Pia vitendo vya kuning’iniza vitu kama mabango ya matangazo mbalimbali kwa kutumia ndege (helikopta ikiwemo) yanaweza kuleta hatari endapo sheria na taratibu zinazohusiana na matumizi hayo hazitazingatiwa.
- Tangazo hili linatolewa kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mkuu chini ya Sheria Namba 80 ya Usafiri wa Anga na kanuni zake zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga nchini zilizowekwa kwa lengo, hususan, kuhakikisha usalama katika matumizi ya vyombo vya usafiri wa anga sambamba na kulinda usalama wa umma na mali wakati wa matumizi ya vyombo husika.
- Watoa huduma za usafiri wa helikopta au ndege na marubani wake wanaokodishwa kutoa huduma wakati wa kampeni, na mtu yeyote anayetarajiwa kutumia huduma hiyo wanakumbushwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafiri wa anga na ikibidi kuomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kanuni zinapatikana kupitia tovuti yetu kwa anuani ya:www.tcaa.go.tz; na endapo utahitaji maelezo ya ziada au miongozo zaidi usisite kuwasiliana na Mamlaka.
- Tangazo
hili linatolewa kwa lengo la kutoa mwongozo kwa watoa huduma za
helikopta, marubani wake na umma kwa ujumla kuhusiana na hatua za
kiusalama zinazopaswa kuzingatiwa inapolazimika kutoa huduma ya usafiri
wa helikopta hapa nchini, hususan, maeneo ya mbali (vijijini) ambapo
huduma za uongozaji ndege hazipo au sio maeneo maalum yaliyotengwa kwa
ajili ya helikopta kutua (mahsusi kwa helikopta au viwanja vya ndege kwa
ujumla). Tangazo hili limetolewa baada ya Mamlaka
kugundua kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya huduma hizi kinyume na
kanuni za usafiri wa anga nchini na weledi unaozingatia taratibu za
kitaaalamu na miongozo katika usafiri wa anga.
- CHETI CHA NDEGE KWA USALAMA WA KURUKA – AIRWORTHINESS CERTIFICATE
- Helikopta yeyote itakayotoa huduma katika kampeni za kisiasa lazima iwe ina cheti halisi cha usalama wa kuruka kilichotolewa na mamlaka husika ya helikopta ilikosajiliwa. Kwa hapa nchini cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga. Na cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa kwa ajili ya helikopta yenye usajili na mahsusi kwa kazi ya kubeba abiria ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine zozote. Kwa tangazo hili helikopta nyingine yeyote ile isiyokuwa na sifa hiyo haiwezi kutumika kufanya biashara ya usafiri wa abiria katika kampeni.
- Endapo helikopta itakuwa ina usajili wa nje ya Tanzania, mtu anayetarajia kuitumia hapa nchini ni lazima apate kibali cha kuiingiza nchini na kuitumia kwa usajili wa nchi iliyotoka kama ilivyoainishwa katika Waraka wa Mamlaka unaoainisha taarifa za usafiri wa anga – Aeronautical Information Circular (AIC 08/09). Hakikisha unapoomba kibali uwe umekidhi vigezo vya waraka huu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nakala za nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa zikiwemo cheti cha usajili wa ndege, cheti cha ndege kwa usalama wa kuruka, cheti cha leseni za radio za ndege, cheti cha bima, makubaliano/mkataba wa kukodisha ndege hiyo, utaratibu wa kufanya matengenezo ya ndege hiyo, leseni za marubani, na ushahidi wa karibuni wa matengenezo ya ndege hiyo.
- TARATIBU ZA USALAMA WA UENDESHAJI
- Mahitaji ya jumla ya kiuendeshaji
Matakwa ya marubani na uendeshaji unatakiwa kufuata maelekezo husika yaliyomo kwenye Kanuni inayohusiana na uendeshaji, yaani, The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Rubani Mkuu anawajibika kuhakikisha kwamba vituo vya Mamlaka vya kuongoza ndege vinavyohusika katika eneo atakalokuwepo au kwa utaratibu wa uongozaji ndege, wanakuwa na taarifa za mpango wake mzima wa safari husika kwa siku au wakati husika.
Njia itakayotumiwa na rubani izingatie matakwa ya kuepuka kuruka chini ya kiwango cha umbali unaotakiwa hasa katika maeneo yenye watu wengi yakiwemo maeneo yaliyopangwa kufanyika kwa mikutano husika.
Tahadhari ni lazima zichukuliwe wakati wa kuelekea kutua, kutua kwenyewe na hata wakati wa kuondoka, hasa ikizingatiwa kuwa kuna uwezekano wa wananchi kuikimbilia helikopta au eneo la utuaji. Katika hali yeyote ile rubani hapaswi kutumia chombo chake kukusanya wananchi kwa ajili ya mkutano au kuitumia kwa utaratibu wowote mwingine kinyume na matakwa ya kiurukaji kwa ndege husika. - Usalama wa eneo la kutua na kuruka
Maeneo yote yatakayotumika kwa ajili ya kutua ama kuruka ni lazima yafahamike mapema. Maeneo ya kuruka ama kutua ni lazima yawe mbali na eneo mkutano utakapofanyika ili kuweza kutoa eneo salama kwa ajili ya kuruka ama kutua kutoka katika mikusanyiko ya watu.
Maeneo ambayo yatatambuliwa kama ni ya kuruka ama kutua hasa yale ambayo hayajatambulika kisheria kwa kufanyia shughuli hiyo ni lazima yawekewe alama maalum na uzio ili kuzuia watu wasiohusika kusogelea eneo hilo.
Eneo husika ni lazima lilindwe; rubani mkuu ahakikishe helikopta itakayokuwa imetua eneo hilo inalindwa dhidi ya uvamizi kutoka kwa watu wasiohusika. Hatua maalum za kiulinzi ni vyema kuchukuliwa endapo kutakuwa na ulazima wa chombo hicho kulala katika eneo husika usiku mzima. Kila wakati rubani anapotaka kuruka ni vyema ahakikishe amekagua chombo chake kwa mujibu wa taratibu zinazohusika kwa umakini kabla ya kuanza safari. - Usiamizi wa Chombo kikiwa ardhini na usalama kwa umma
Mtu mwenye wajibu wa usimamizi wa chombo kikiwa ardhini lazima awe ni mwenye mafunzo ya kutosha na awe anajua madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanapozunguka. Kwa marejeo zaidi kuhusiaha na hilo tafadhali zingatia yaliyomo kwenye Waraka wa Mamlaka AIC33/2000 unaoelezea masuala ya madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanayozunguka.
Ni wajibu wa Rubani mkuu na mhusika aliyekodisha helikopta kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na mbali na helikopta. Matumizi ya kizembe na yasiyo ya kiweledi ya helikopta yatakayohatarisha usalama wa wananchi yatachukuliwa kama ukiukwaji wa kanuni za usafiri wa anga na Mamlaka itawachukulia hatua kama ilivyoanishwa kwenye kanuni hizo. - Kuchukua na kuangusha vitu ardhini na kupeperusha mabango angani
Huduma hizi zinaweza kufanywa na helikopta na hata ndege zingine za kawaida. Kabla ya kufanya shughuli za namna hiyo, mmiliki wa chombo ni lazima ahakikishe anakidhi vigezo vya Kanuni za Usafiri wa Anga kwa huduma hizi, yaani, The Civil Aviation (Aerial Work) Regulations na pia awe amepatiwa kibali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga kwa kazi hiyo. Mmiliki wa ndege yeyote anayefanya shughuli za namna hii bila ya kuzingatia vigezo vya Kanuni hizi atachukuliwa hatua. - Kutoa taarifa za matukio
Rubani Mkuu ni lazima aandike taarifa ya matukio na kuiwasilisha Mamlaka ya Usafiri wa Anga kama ilivyoanishwa kwa mujibu wa kanuni za usafiri wa anga hususan, kanuni za 52, 74,75 na 76 zilizomo kwenye Kanuni ya The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Wananchi nao wanatakiwa kutoa taarifa ya tukio lolote waliloliona hatarishi kwa mujibu wa kanuni namba 262 ya Kanuni iliyotajwa.
Mamlaka itafuatilia na kuchunguza taarifa inazozipokea na kuchukuwa hatua stahiki ili kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa kiuendeshaji, watu na mali.
- Mahitaji ya jumla ya kiuendeshaji
- HITIMISHO
Ili kulinda usalama wa wananchi, wamiliki na marubani wote wanapaswa kuhakikisha wanazingatia Sheria ya Usafiri wa Anga pamoja na Kanuni zake. Rubani anayeendesha chombo ni lazima ahakikishe anatumia weledi wa hali ya juu katika matendo yake.
Mamlaka inawahakikishia wananchi/umma kwa ujumla kwamba haitosita kuchukuwa hatua stahiki kama zilivyoanishwa kisheria na kanuni za usafiri wa anga iwapo mapungufu ya usalama yatajitokeza.
Imetolewa na
Charles M. Chacha
Kaimu MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA
Ukweli Unauma: Jiwe walilolikataa CCM limekuwa jiwe kuu Chadema
By Padri Baptiste Mapunda
Katika hatua hii ya Mzee Lowassa kukihama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na chama kikuu cha upinzani nchini, anaonekana kuhama na baadhi ya vigogo wa CCM. Na sasa ukweli unaanza kujitokeza juu ya uhai, uimara, mpasuko, udhaifu na upungufu ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.
Injili inatufundisha kuwa enzi ya Yesu Kristo, baadhi ya watu walimwona ni kama kichaa na mvuruga amani katika jamii.
Wengine
walimdharau hata kufikia hatua ya kusema “ huyu tunamjua, je, siyo
mwana wa Yusufu na Mariamu?” Hata hivyo, Yesu aliendelea na kazi ya
kuwaletea binadamu ukombozi.
Wakati
viongozi wakuu, wasomi na maadui zake wakimtuhumu kwa utovu wa nidhamu,
dhambi na mambo mengine, watu wa kawaida walizidi kumiminika na
kumfuata.
Watanzania
wa leo na hasa wanasiasa hawapendi kutumia maandiko matakatifu
yanayopingana na matakwa yao au sera zao.Wanasiasa hupenda kutumia
maandiko yale yanayotetea nafsi zao,masilahi yao na madaraka yao.
Mfano
wa hili ni yale maandiko yasemayo: ‘’kila kiongozi anatoa mamlaka kwa
Mungu kwa hivyo ni lazima kuyatii.” Lakini ukweli ni kwamba maneno ya
Mungu ukiyatumia vibaya ni wazi lazima yatakuja kukugeuka muda si mrefu.
Kwa
sababu maandiko matakatifu hasa Biblia ina majawabu yote yanayotafutwa
na mwanadamu kwa sababu yanahusu historia ya mwanadamu na Mungu jinsi
walivyotembea pamoja.
Ukitaka
kujua kama unaendelea au la au upo sahihi katika mambo fulani ni lazima
ulinganishe na mtu au kitu kingine au tukio fulani. Ukisikiliza hukumu
za kesi mbalimbali utasikia hakimu ananukuu hukumu ya kesi iliyofanyika
nchi fulani na hivyo kuifanya kama msingi wa hukumu anayoitoa. Wataalamu
wanasema ‘hakuna jipya chini ya jua.’
Uchaguzi wa mwaka huu
Sasa
tukirudi katika ulingo wa siasa za Tanzania na yanayotokea nyakati hizi
hususani uchaguzi wa mwaka huu, tusifikiri ni tukio ambalo halijawahi
kutokea popote duniani. La hasha! itakuwa ni kujidanganya. Siyo siri
kwamba tangu waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ahame CCM na kujiunga
na Chadema, siasa za Tanzania zimebadilika, hili halina upinzani.
Sijui
kama CCM walitabiri madhara ya kulikata jina lake mapema katika vikao
vya juu vilivyofanyika kule Dodoma au na wao wanashangaa kama mimi.
Sasa
hivi mazungumzo nchini Tanzania karibu kila kona ni Lowassa. Nilikwenda
kuona wagonjwa hospitalini, nilikuta baadhi ya wagonjwa na mfanyakazi
mmoja wakiwa katika mjadala mzito juu ya Mzee Lowassa. Mfanyakazi mmoja
wa hospitalini hapo alitaka kupindisha ukweli, alipewa ukweli wake na
wagonjwa waliokuwa karibu.
Walimwambia: “ Hatutaki kudanganywa kwani Lowassa kwa CCM kawa fisadi kwa vile ameondoka?”
Hii ni alama wazi kwamba wananchi sasa wameanza kujitambua na kutambua
kile kinachoendelea katika siasa zetu ikiwamo propaganda na porojo za
kisiasa.
Ukweli
ni kwamba kinachoonekana katika siasa za Tanzania kinalinganishwa na
kilichotokea katika maisha ya Yesu. Alifanyiwa kila aina ya fitina,
chuki, mizengwe hata akasalitiwa na rafiki yake Yuda na hatimaye akauawa
kwa kutundikwa msalabani.
Kwa
baadhi ya watu Yesu alionekana ni mzushi, alikuwa mchochezi katika
jamii, alikuwa mvunja sheria za Wayahudi na mtu aliyekuwa anahatarisha
amani ya jamii. Kuna mahali alifika akamponya mtu mwenye pepo kisha
nguruwe wakaswagwa baharini.
Mzee
Lowassa kajiondoa CCM na sasa amegeuka kuwa lulu na kivutio ndani ya
Chadema, Ukawa na kwa Watanzania kwa jumla. Kwa mantiki hii kweli mzee
Lowassa anaonekana kuwa kama jiwe lililokataliwa ndani ya CCM, lakini
sasa limekuwa jiwe kuu ndani ya Ukawa.
Mzee
Lowasa analaumiwa kuwa amekuwa akihonga ili watu wamuunge mkono katika
harakati zake. Lakini kwa upande wangu ninashangaa kwani kadiri siku
zinavyopita, watu wanaomuunga mkono wanaongezeka. Najiuliza hivi Lowassa
ana fedha kiasi gani kuthubutu kuuhonga ule umati uliokusanyika Dar es
Salaam, Mbeya, Arusha na hatimaye mjini Mwanza ?
Hakuna
mtu au kiongozi aliyelaaniwa hapa duniani na kuchafuliwa, kutukanwa,
kudharauliwa na kusiginwa kama Yesu mwana wa Yusufu, lakini hata hivyo
watu kila siku alipokuwa anakwenda walikusanyika mamia kwa mamia kinyume
cha matakwa ya maadui zake.
Najiuliza
wale wote wanaomfuata Lowasa ni wehu, vichaa, wajinga na wapumbavu?
Kufikiri hivi itakuwa ni makosa na kujidanganya, itakuwa ni kutafuta
majibu mepesi kwa maswali magumu. Kuleta porojo katika jambo nzito kama
hili ni kujiaibisha mbele ya umma.
Huku ni kumfanya Mzee Lowassa aonekane kama ‘ jiwe lililokataliwa ndani ya CCM na sasa limeguka kuwa jiwe kuu ndani ya Ukawa.”
Katika hatua hii ya Mzee Lowassa kukihama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na chama kikuu cha upinzani nchini, anaonekana kuhama na baadhi ya vigogo wa CCM. Na sasa ukweli unaanza kujitokeza juu ya uhai, uimara, mpasuko, udhaifu na upungufu ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.
Kwa
mantiki hii utabiri wa Mwalimu Julius Nyerere juu ya upinzani wa kweli
kutoka ndani ya CCM yenyewe, unaendelea kutimia siku hadi siku.
Kwa upande wangu, nazidi kupata nguvu ya kuandika kwamba ‘CCM imegeuka mnara wa Babel’.
Thursday, 20 August 2015
Mheshimiwa Edward Lowassa asaini hati ya kiapo mahakama kuu ya kugombea Urais wa Tanzania
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa
akisaini fomu za hati ya kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya
Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Hati ambayo kila
mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini
Dar es Salaam Kushoto ni Mgombea Mwenza, Juma Haji Duni.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akisaini fomu za hati ya Kiapo kwenye ofisi za Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2015. Kushoto kwake ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akipokea fomu za hati ya Kiapo kutoka kwa Jaji wa Mahakama ya Tanzania, Jaji Suleiman Said Komu. Kulia ni Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa.
Wednesday, 19 August 2015
ORODHA YA MAJINA YA WANACHAMA WA CHADEMA WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
ORODHA YA MAJINA YA WANACHAMA WA CHADEMA WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE
Subscribe to:
Posts (Atom)





















