Monday, 3 August 2015

Lowassa arejesha fomu ya kugombea Urais CHADEMA

 Mh. Edward Lowassa amerejesha fomu ya kugombea urais CHADEMA na mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti bara wa CHADEMA Prof Abdallah Safari amepokea fomu hizo.

Prof Safari amesema mpaka sasa hakuna mgombea yoyote wa Chadema zaidi ya Mheshimiwa Edward Lowassa aliyechukua fomu ya kugombea Urais

Mheshimiwa Edward Lowassa amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1 na laki 6.
 Mwanasheria wa Chama Mh Mabere Marando akikagua fomu za mgombea urais Mh. Edward Lowassa mara baada tu ya kukabidhi kwa Makamu Mwenyekiti Bara Prof Abdalah Safari

Makamu Mwenyekiti akipokea fomu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu na aliiyekuwa mbunge wa Monduli kwa tikeki ya CCM Mh. Edward Lowassa
Baadhi ya wabunge walioweza kufika katika tukio la kumshuhudia Edward Lowassa akirudisha fomu Makao Makuu 
 Ester Bulaya akiwa ukumbini kumshuhudia Edward Lowassa akirudisha fomu ya kugombea urais ndani ya chama
 Baadhi ya wananchi wakiwa na ujimbe kwenye mabango yao,ikiwa ni sehemu ya kufikisha ujimbe kwa wazo la kila mtu binafsi kwa kupata fursa ya kutoa mawazo yao kwa njia ya mabango
Suzan Lyimo Mbunge viti maalum CHADEMA akisalimiana na Mh Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Makao Makuu kurudisha fomu ya kugombea urais kupitia CHADEMA

No comments:

Post a Comment