Monday, 17 August 2015

PICHA ZAIDI ZA TUKIO LA MKUTANO MKUBWA WA KUMTAMBULISHA MGOMBEA WA UKAWA NDUGU EDWARD LOWASSA MWANZA

 Mgombea Urais kupitia UKAWA ndugu Edward Lowassa akiwa na Mgombea mwenza ndugu Juma Duni Hajii katika wa mkutano wa kumtambulisha jijini Mwanza
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, Jijini humo, leo Agosti 16, 2015.


 Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza wakati wa kumtambulisha Mgombea wa UKAWA jijini Mwanza

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa wagombea hao na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.

 Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi katika Barabara kuu ya kutoka Uwanja wa Ndege kuelekea katikati ya mji, wakati wa mapokezi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,ambaye yupo kwenye ziara ya kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, leo Agosti 16, 2015.
Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, kulikofanyika Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.

No comments:

Post a Comment