Monday 3 August 2015

Mkutano wa Baraza kuu CHADEMA .....unaendelea

Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati.

Mbowe-Tulilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi.

Mbowe-Tuliridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama chetu ni mpango wa Mungu.

Mbowe-Umoja wetu ndio ushindi, fursa iliyojitokeza ni nadra.

Mbowe-Mtikisiko huu umekuja kwa CCM kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko

Mbowe-Hatuwezi kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho

Mbowe- Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu tuanze siasa za vyama vingi

Mbowe-Kila tunayeweza kumpokea kutoka vyama vilivyo nje ya UKAWA tutamchukua

Mbowe-Mungu ameamua kutumia chama chetu kujeruhi na kuangusha CCM.

Mbowe-CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, chama makinI ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.







No comments:

Post a Comment