Tuesday 4 August 2015

Mwenyekiti wa Wenyeviti CCM Taifa, Mgana Msindai Ahamia CHADEMA


Mwenyekiti wa wenyeviti ccm Taifa na mwenyekiti wa mkoa wa singida Mhe Mgana Msinda  akiwasalimia  wajumbe  wa  Baraza  Kuu CHADEMA **** Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai jana alijiunga na Chadema na kutambulishwa katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema.
 

Mgana, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Iramba Mashariki (2000-2010) alitambulishwa pamoja na Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Goodluck Ole Medeye na ofisa mwandamizi wa chama hicho, Matson Chizii.
 
Makada hao wa CCM jana usiku waliambatana katika kikao hicho na aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowassa. 
 

Habari zinasema kuna makada zaidi wa CCM watakaotambulishwa katika mkutano mkuu wa Chadema leo.

No comments:

Post a Comment